Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Diamond Platinumz,  Hamis Taletale maarufu kama ‘Babu Tale’,  ametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani na jeshi la polisi kwa amri ya Mahakama kuu jijini Dar es salaam.

Babu Tale anashikiliwa kwa kesi ya madai ya Shilingi Milioni 250 ambapo kipindi cha nyuma Mahakama ilimwamuru Babu Tale amlipe fedha hiyo Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde mara baada ya kukamatwa na hatia ya ukiukaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo ya Sheikh huyo kibiashara bila ridhaa yake.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi,  katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyomlalamikia Babu Tale na ndugu yake Iddi Tale.

Tayari Babu Tale amefikishwa mahakamani kusikiliza kesi ya madai inayomkabili.

Maalim kufanya mahojiano mubashara na waandishi wa habari
Mdee amuibua Kairuki bungeni sakata la kifuta jasho kwa waliotumbuliwa