Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo bado haijafahamika ameachiwa kwa dhamana au vinginevyo.

Tale alifikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake inayomkabili akishitakiwa kushindwa kulipa deni analodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo  yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

Ulimwengu asepa Ulaya arudi Afrika kisoka
Pochettino kubaki Spurs mpaka 2023