Msanii wa nyimbo za bongo fleva, Hawa Mayoka maarufu kama Hawa aliyepata umaarufu kupitia wimbo wa Nitarejea aliouimba na msanii mkubwa nchini, Diamond Platinumz yupo nchini India kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa unaomsumbua.

Ambapo madaktari nchini India wamesema asilimia 95% hawajaona tatizo linalohusiana na ini ila ni moyo ndiyo uliokuwa unamsumbua na kupelekea mwili wake kujaa maji.

Wataalamu hao India wamesema Hawa atahitajika kufanyiwa upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa.

”Baada ya kuwasili India msanii wa Bongo fleva Hawa Mayoka ‘Hawa wa Nitarejea hajakutwa tatizo la ini kama ilivyoripotiwa wakati akitibiwa hapa nchini, bali amebainika ana tatizo la moyo  linalofanya tumbo lake kujaa maji kila wakati” Babu Tale.

Taarifa hizo zimetolewa na Meneja wa Diamond, Babu Tale ambaye ndiye amesimamia zoezi zima la kumsafirisha Hawa nchini India kwa ajili ya matibabu mara baada ya msanii wake Diamond kujitolea kugharamia matibabu yake kwa kumchangia Milioni 50.

Hawa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbo pamoja na miguu kujaa maji ambapo madaktari nchini walibainisha kuwa anatatizo la ini.

Aidha Babu Tale amewaomba watanzania kuendelea kumuombea Hawa kwani anaingia kwenye upasuaji mkubwa vile vile waendelee kumuombea Diamond aendelee na moyo wa kujitoa kumsaidia Hawa aweze kufanikisha matibabu yake.

 

Swagz avenue kusaini mkataba na Kanye west
Lema ajisalimisha kituo cha polisi

Comments

comments