Mabingwa wa soka nchini Kenya, GOR MAHIA FC wamethibitisha wameshindwa kumzuia beki wao tegemeo, Joash Onyango asijiunge na na mabingwa wa Tanzania bara Simba kutokana na suala la kimslahi.

Beki huyo ambaye amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ubishi juu ya umri wake wa miaka 27, takwimu za pasi yake ya kusafiria zinaonyesha amezaliwa 1993.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka la Kenya, Simba imeokota dodo kutokana na umahiri na uzoefu wa mchezaji huyo, kwani mkataba wake na Gor Mahia ulishamalizika na anatua Msimbazi kama mchezaji huru, jambo litakalowapunguzia Simba gharama.

Wanasema mchezaji huyo si Babu kama wanavyotafsiri mashabiki wa Bongo kwani, ni staili yake ya kawaida ya kupaka rangi nyeupe ndevu zake.

Gor Mahia imeandika kwenye mtandao huo kuwa Onyango huenda akasaini dili ya miaka miwili muda wowote kuanzia sasa, kwa kuwa wameshaafikiana kuhusu maslahi binafsi.

Onyanyo, ambaye ni beki tegemeo kwenye timu ya Taifa ya Kenya *Harambee Stars* alijiunga na Gor Mahia mwaka 2017 akitokea Western Stima na kushinda mataji kadhaa.

Msimu wa 2018/19 alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu nchini kwao Kenya.

Gor wameshindwa kumzuia kutokana na hali ngumu ya kifedha iliyopo klabu hapo kwa sasa n wameona ni bora kumuachia ili akatafute changamoto mpya ya soka lake, na sasa imedhihirika anatua Msimbazi.

Tayari televisheni ya Citizen ya Kenya imeshantaza rasmi taarifa za beki huyo kujiunga na Wekundu Wa Msimbazi Simba, ambao msimu ujao wamedhamiria kufanya vyema kwenye michuano ya Tanzania bara na ile ya kimataifa.

Kwa mantiki hiyo  Onyango anajiunga na Meddie Kagere na Francis Kahata ambao, walicheza pamoja Gor Mahia.

Onyango alipoulizwa kuhusu mpango wa kuja Tanzania aligoma kufafanua lolote kuhusu dili lake na Simba kwa madai bado hajakamilisha baadhi ya mambo.

Simba ambao jana walikuwa bize wakihangaika na hukumu ya Bernard Morrison, wanasuka upya safu yao ya ulinzi kujiweka sawa kwa Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu.

Msumbuji yapokea uenyekiti wa Baraza la mawaziri SADC
Watoa huduma za afya watakiwa kuzingatia maadili