Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo na kutengwa kwa asilimia tano ya fedha za Bahati Nasibu kumesaidia kwa kiwango cha maendeleo ya michezo nchini.

Kauli hiyo ameitoa mapema hii leo Machi 16, 2022, jijini Dodoma, alipokuwa akieleza mafanikio ya wizara yake kwa kipindi cha mwaka mmoja cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani.

Waziri Mohamed Mchengerwa.

“Hadi Februari mwaka huu kiasi cha TZS Bilioni 1.55 kimepokelewa kutoka Hazina. Fedha hizi zimeanza kusaidia maendeleo mbalimbali ya michezo nchini na zitasaidia pia katika programu za uendelezaji wa miundombinu.” alisema Mchengerwa.

Pamoja na hayo Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja, serikali imekamilisha hatua muhimu za ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo kukamilika usanifu wa uwanja wa soka wa Dodoma, kukamilika usanifu wa ujenzi wa viwanja vya mazoezi na kupumzikia wananchi vitakavyojengwa  Dar es Salaam, Dodoma na Geita.

Picha ya uwanja wa michezo Dodoma

Akiyataja mafanikio mengine ya wizara, alisema kuwa jumla ya pesa za Kitanzania Bilioni 19 zitatumika kukarabati shule zisizopungua 58 za michezo na kuwekewa miundombinu mbalimbali ya kisasa.

Waziri Mchengerwa alisema kuwa nchi ya Tanzania, Novemba mwaka 2021 ilipata bahati ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Soka kwa Walemavu Afrika (CANAF-2021) ambapo pamoja na kupokea takribani nchi 13 kutoka Afrika, Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Walemavu, ‘Tembo Warriors’, ilikuwa miongoni mwa Timu nne zilizofuzu kutoka Afrika kwenda Kombe la Dunia Uturuki Oktoba mwaka huu.

Amuua mkewe na mtoto
Diamond Plutnums alia na BASATA