Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango ameeleza kuwa Ukuaji wa Pato halisi la Taifa unatarajiwa kupungua kutoka makadirio ya awali ya 6.9% na kufikia 5.5% mwaka 2020 kulinganishwa na 7% mwaka 2019.

Amesema hii ni kutokana na athari za ugonjwa wa COVID-19 ulioenea katika nchi nyingi ambazo ni washirika wakubwa wa kibiashara wa Tanzania.

Amesema hadi Aprili 2020 deni la Taifa limefikia Shilingi za Kitanzania, Trilioni 55.43 ambapo Kati ya hilo, deni la nje ni trilioni 40.57 na ndani ni trilioni 14.85. Aprili 2019, Deni hilo lilifikia TZS trilioni 51.03.

Kwa upande wa pato la wastani kwa kila mtu mwaka 2019 lilikuwa sh. 2,577,967 kulinganishwa na sh. 2,452,406 mwaka 2018.

Hata hivyo amesema Serikali inaendelea kuchuka hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa wa covid 19 ambapo hadi sasa imetoa sh. bilioni 15.9 kwaajili ya ununzi wa vifaa tiba na kinga.


Manara: Tutafikisha alama 100 VPL, tutatwaa ubingwa ASFC
JPM 'awajibu' wanaopanga kumuongezea muhula wa tatu madarakani