Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Bukoba mkoani Kagera, limepitisha bajeti ya zaidi ya shilling bilioni 50.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2019-2020.
 
Akisoma rasimu ya bajeti hiyo katika baraza la madiwani, Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Julian Tarimo amesema kuwa vipaumbele vilivyolengwa kuwa ni afya, elimu, maji na miundombinu pamoja na mambo mengine na kuwataka madiwani hao kuipitisha bajeti hiyo kwa kuwa inalenga maslahi ya wananchi.
 
Amesema kuwa fedha hiyo ni pamoja na mapato ya ndani ikiwemo pia fedha kutoka serikali kuu ambayo inalenga kumalizia miradi viporo lakini pia kuanzisha miradi mipya ambayo itakuwa na tija kwa wananchi.
 
Aidha, katika bajeti hiyo kiasi cha shilingi milioni 260 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa shule ya sekondari Rukoma itakayoanzishwa katika kata Rukoma ili kuwapunguzia adha ya kutembea wanafunzi waliokuwa wakisafiri mwendo mrefu wa zaidi ya km 15 wakifuata masomo.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Bukoba, Deodatus Kinawiro ameshauri bajeti hiyo kuwa chachu ya maendeleo hasa kujikita katika kufufua zao la chai ambalo limeonekana kupotea mkoani Kagera na kuongeza kuwa kiwanda cha chai kina uwezo wa kuchakata tani 60 kwa siku na sasa kinachakata tani 7 hadi 8 kutokana ukosefu wa zao hilo.
 
  • Ole Sendeka atoa maagizo,’ Sasa kuanza na wenyeviti’
  • RC Songwe awashukia TBA kuhusu ujenzi wa nyumba za serikali
 
  • Sakata la CAG, Spika Ndugai Mahakama yatoa uamuzi
 
Naye Mwnyekiti wa halmashauri hiyo, Murshidi Ngeze ambaye pia ni diwani wa kata ya Rukoma ameelezea namna walivyojipanga kuhakikisha fedha za serikali zinafanya kazi iliyokusudiwa hasa katika miradi ya elimu afya na maji pamoja na 4% ya mapato ya ndani kwenda kwa vijana, 4% kwenda kwa wanawake na 2% kwenda kwa walemavu

Watendaji wapewa onyo kali ugawaji wa vitambulisho awamu ya pili
Mwanajeshi aliyetoroka jela yenye ulinzi mkali arejea nyumbani