Mchezaji wa Real Madrid na raia  wa Wales, Gareth Bale ameendeleza utawala wake wa kujishindia tuzo ya Mchezaji Bora wa Wales kwa mara ya nne mfululizo, nyota huyo wa Real Madrid amepewa heshima hiyo kufuatia sherehe zilizofanywa na Chama cha Soka nchini humo jana.
 Bale, 27, aliiongoza Wales kwa mafanikio kwenye Michuano ya Euro 2016 na kufanikiwa kufika hatua ya nusu fainali akifunga mabao 3 katika hatua ya makundi, huku akishinda taji la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili akiwa na Real Madrid.
Hata hivyo Bale amecheza  mechi 64 kwenye taifa lake mpaka sasa, ambapo hivi karibuni amesaini mkataba mpya na timu yake ya Real Madrid, pia ananyemelea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo akibakisha magoli matatu tu kuivuka rekodi ya Ian Rush aliyefunga mabao 28.
Trump: mimi ni Rais wa wamarekani wote
Rais Magufuli ampongeza Trump kwa ushindi, amhakikishia hili