Kiungo kutoka nchini Uganda, Taddeo Lwanga amewapa neema wachezaji wote wa Simba SC, kwani bao lake ambalo alifunga katika mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Young Africans, limekua kichocheo cha kikosi cha Simba kupewa mkwanja wa Shilingi 200 Milioni kama bonasi.

Mkwanja huo utaingia kwenye akaunti za wachezaji wote wa Simba SC, muda wowote kabla ya mwishoni mwa juma hili, na hiyo ni kwa mujibu wa viongozi wa klabu hiyo ya Msimbazi.

Inaelezwa katika bonasi hiyo kila aliyecheza hata dakika moja kama Bernard Morrison hatapata chini ya Shilingi 10 Milioni na ambaye aliishia benchi bila kucheza kama kipa Benno Kakolanya watapata si chini ya Shilingi 6 Milioni wakati wale ambao walikuwa jukwaani kama Said Ndemla watapata si chini ya Shilingi 3 Milioni.

Simba SC imemaliza Msimu wa 2020/21 kwa mafanikio makubwa ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo na Kombe la Shirikisho (ASFC) mara mbili mfululizo, huku ikiishia hatua ya Robo Fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mo aweka mzigo, kujenga uwanja
Tatizo la maji Mkoa wa Pwani kubaki historia