Mshambuliaji Super Mario Balotelli, amefanikisha azma ya kurejea nyumbani na kujiunga tena na klabu ya AC Milan akitokea nchini England alipokua akiitumikia klabu ya Liverpool.

Balotelli amerejeshwa AC Milan kwa mkataba wa mkopo na jana alifanyiwa vipimo vya afya dakika chache mara baada ya kuwasili mjini Milan akitokea jijini Liverpool nchini England.

Baada ya kufanyiwa vipimo, moja kwa moja mshambuliaji huyo aliungana na wachezaji wengine katika mazoezi ya AC Milan na alionekana kuwa mwenye furaha baada ya kukutana na rafiki na jamaa zake ambao aliwaacha klabuni hapo mwaka 2014 baada ya kusajiliwa na Liverpool kwa ada ya paund million 16 mwanzoni mwa msimu uliopita.

Balotelli ameahidi kusaidiana na wenzake kikamilifu na anaamini nafasi ya kurejea klabuni hapo inamfungulia mipango mipya katika maisha yake ya soka ambayo mara kadhaa yamekua yakitawaliwa na misukukosuko.

Amesema jukumu lake ni kucheza soka, na ameshajitambua nini anachotakiwa kufanya, hivyo amewaahidi mashabiki wake pamoja na wale wa AC Milan kusubiri kumuona akiwa katika jukumu la kutimiza malengo yanayokusudiwa huko San Siro.

Viongozi wa AC Milan walikubaliana mwishoni mwa juma lililopita, kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkopo baada ya kuona mambo yanamuendea kombo akiwa ugenini England.

Hata hivyo mtendaji mkuu wa AC Milan, Adriano Galiani alisema nafasi ya kusajiliwa kwa mkopo kwa mshambuliaji huyo itakua ni ya mwisho kutokana na utovu wa nidhamu ambao wamekua akiuonyesha mara kwa mara.

Lakini kiongozi huyo aliahidi huenda wakamsajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu huu, endapo Balotelli ataonyesha uwezo mkubwa wa kisoka na kuachana na mambo ya kipuuzi ambayo amekua akiyafanya.

Stones Awasilisha Ombi La Kuondoka Goodson Park
Magufuli Alia Na Wala Rushwa, Pinda Amuongezea Nguvu