Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amekabidhi jumla ya sh. bilioni 1.040 kwa Waziri Mkuu, Majaliwa kwaajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika Septemba 20, 2016 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam ambapo Balozi Kijazi amesema kiasi cha sh. 1,000,030,100 kimekusanywa kutoka kwa watumishi wa idara na Wizara zote za Serikali na kwamba michango zaidi bado inaendelea kukusanywa.

“Tunaamini michango hii itasaidia kuwafuta machozi wenzetu waliopatwa na maafa japokuwa tunajua haitatosha kurudisha kile walichopoteza. Tuna imani itasaidia kupunguza makali ya machungu waliyoyapata,” – Balozi Kijazi.

Balozi Kijazi pia amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba bado wanaendelea kukusanya michango kutoka kwenye Idara na Wizara nyingine ambazo zilichelewa kupata taarifa na kwamba wakikamilisha wataiwasilisha mapema iwezekanavyo.

Cesc Fabregas: Nimewaziba Midomo Waandishi Wa Habari
JPM atengua uteuzi wa Prof. Mlawa LAPF, Avunja Bodi