Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameapa kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na kulisihi Bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu  na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameapa kuwa mjumbe wa maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA). Balozi Mulamula ameapa kuwa mjumbe wa maamuzi wa AELA leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam. Picha na Mambo ya Nje. 
Waziri Mkuu atoa agizo Halmashauri za Dodoma
RC Makalla ataka fedha za TASAF ziwafikie wahusika