Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambaye leo ameshuhudia mrithi wake, Balozi John Kijazi akila kiapo mbele ya Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, ametoa neno lake la moyoni.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya tukio hilo la kiapo, Balozi Sefue amemshukuru Rais John Magufuli kwa kile alichodai kuendelea kufanya nae kazi wakati ambapo muda wake ulikuwa umekwisha.

“Namshukuru sana Rais Magufuli… hakuwa na lazima ya kuendelea na mimi. Lakini akaona kwamba kwenye kipindi hiki cha mpito naweza kumsaidia,” alisema

“Kwa hiyo na yeye namshukuru sana, najisikia naheshimika sana kuwa pembeni yake kwa kipindi hiki cha serikali ya awamu ya Tano,” aliongeza.

Kadhalika, Balozi Sefue alimshukuru Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete aliyemtoa Marekani alipokuwa akifanya kazi, na kumpa nafasi ya kuwa Katibu Mkuu Kiongozi nchini.

Sakata la kusimamishwa Wauguzi Butimba, madaktari wagoma
Mkwasa Kutangaza Kikosi Cha Taifa Stars