Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa Dk Ali Mohammed Shein (CCM) na Maalim Seif (CUF) wamekubaliana kurudia uchaguzi visiwani humo kufuatia mazungumzo yanayoendelea.

Akiongea katika mahojiano na redio ya visiwani humo, Makamo huyo wa pili wa rais alieleza kuwa kinachoendelea sasa katika vikao vinavyowahusisha viongozi wa pande mbili ni kuhusu Tume itakayosimamia uchaguzi huo.

“Kimsingi tumeshakubalina kurejewa kwa uchaguzi ila mazungumzo yayoendelea sasa ni kuhusu tume itakayosimamia uchauguzi huo kama ni hii chini ya mwenyekiti Jecha Salim Jecha au kuundwa nyigine,” anakaririwa.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Balozi Seif imepingwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Nassor Ahmed Mazrui ambaye amesema kuwa mazungumzo yanaendelea lakini bado kuna mvutano mkubwa kwa kuwa Maalim Seif ameendelea kushikilia msimamo wake na wa chama chake kuwa uchaguzi usirudiwe.

“Sio kweli, CUF haijakubali na haitakubali kurejewa kwa uchaguzi kwa sababu uchaguzi ulishafanyika Oktoba 25 na ulikuwa huru na haki,” alisema.

 

Millard Ayo Aeleza Alivyowahi kudata Kimapenzi Kwa Jokate
Marekani yatishia kusitisha msaada kwa Tanzania, yatoa masharti kuhusu Zanzibar na Kesi za Makosa ya Mtandao