Graham Stuart aliyekuwa mgeni rasmi katika mechi ya fainali ya Sportpesa super cup kati ya Gor Mahia na AFC Leopards uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ameendelea kusifu ukarimu na upendo wa watanzania aliouona hapa nchini.

Stuart ametumia kurasa zake za twitter kusifu waandaaji wa michuano hiyo Sportpesa kuandaa michuano hiyo pia kuwapa mwaliko maalumu Everton kuja Tanzania ikiwa ni mara yao ya kwanza.

”Ni zaidi ya ushindani uwanjani. Ni nchi ya watu wakarimu na kila mmoja unamuona yupo na hamu kubwa kuishuhudia timu yangu ikicheza pale julai.” ametweet Stuart.

Taarifa mbalimbali zinazotolewa na balozi huyo zinawapa furaha waandaaji wa mchezo huo, Sportpesa pia kuitangaza Tanzania kimataifa kama kisiwa cha amani na kitovu cha ukarimu duniani.

Everton wanatarajiwa kuwasili nchini kesho na ndege toka England mpaka hapa nchini kwa ajili ya mchezo wao na Gor Mahia julai 13.

Maandalizi ya mchezo huo yameshakamilika kama alivyobainisha mkurugenzi wa utawala na utendaji wa kampuni ya Sportpesa nchini Abbas Tarimba.

Tayari viingilio vya mchezo huo vimetangazwa, kwa kawaida ikiwa ni shillingi 3000 za kitanzania na VIP ni shilingi 8000 za kitanzania.

 

Video: Siwezi kustaafu uanachama wa CCM mpaka Mungu anichukue-Mkapa
TCAA yapiga marufuku kununua, kurusha ‘drones’ bila kibali maalum