Mshambuliaji kinda wa klabu ya Chelsea, Patrick Bamford amefupisha mkataba wake wa mkopo wa kuitumikia klabu ya Crystal Palace ambayo alistahili kuichezea kwa  msimu mmoja.

Bamford, 22, ametangaza uamuzi wa kurejea Chelsea kabla ya mkopo wake kumalizika baada ya klabu hiyo kutoka sare ya 0-0 na Swansea Jumatatu.

Imebainika tayari alikuwa amemjulisha meneja wake Alan Pardew.

“Hiyo ilikuwa mechi yangu ya mwisho Palace,” alisema. “Kusema kweli, kimekuwa kipindi kibaya. Hakuna mchezaji apendaye kukaa benchi bila kuchezeshwa.

“Huo ulikuwa uamuzi wangu. Bosi wangu hajazungumza nami.”

Bamford, anayechezea timu ya taifa ya England ya wachezaji wa umri wa chini ya miaka 21, hajaacha kwenye mechi yoyote Ligi ya Premia tangu awasili Palace kutoka Chelsea.

Amecheza mechi tano ligini kama nguvu mpya.

Mechi pekee mbili alizoanza kikosini zilikuwa za Kombe la Ligi.

Bamford alipoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya kuingia kama nguvu mpya dhidi ya Swansea Jumatatu. Aligonga mpira kuelekea kwa kipa Lukasz Fabianski akiwa hatua 12 kutoka kwenye goli.

Steven Naismith Kuondoka Goodson Park
Tajiri Kijana Aipasua Simba Kwa Kauli Tata