Diwani wa kata ya Sombetini Arusha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ally Bananga amewataka madiwani waliopo ndani ya chama chao wanaotaka kuondoka waondoke mara moja kwani wakija kuwagundua kipindi cha uchaguzi kwamba ni wasaliti watawatawanya viungo.

Ameyasema hayo mara baada ya wimbi kubwa la madiwani mkoani Arusha kuhama chama hicho kwa tuhuma za kupokea rushwa, ambapo amesema kuwa anaamini kwamba hakuna tatizo la madiwani kuhama vyama.

Amesema kuwa kuhama ni hiari ya mtu na wanafanya hivyo kwa maslahi yao lakini wasiondoke kwa kununuliwa kwani haitakuwa busara na mwisho wa siku itakuwa ni matatizo kwao.

“Sina tatizo kwa madiwani kuhama hata kidogo, lakini kama ni kuhama kwa kununuliwa kama hivi tunavyoona hili ni tatizo. Kama huna imani yetu ondoka mapema kwa amani. tupishe kwa sababu tunaelekea kwenye uchaguzi na tunaamini tutashinda kata zote, sasa isije ikatokea mbeleni tukakugundua kwamba wewe ni msaliti maana tutatawanyana viungo kitu ambacho siyo kizuri. Ondokeni kwa amani yote sasa hivi mapema,”amesema Bananga

Hata hivyo, ameongeza kuwa anaamini kuwa watashinda katika uchaguzi mdogo kwani wamekuwa bora chini ya uongozi wa Mbunge, Godbless Lema na Meya, Calist Lazaro na kutokana na ushahidi wa Nassari kuonyesha wabunge walikuwa wakinunuliwa kama maandazi safari wamejiandaa kupeleka keki kwenye chaguzi.

Sadio Mane kurejea uwanjani mwezi disemba
Arjen Robben astaafu kwa kufunga mawili