Kikosi cha klabu ya Young Africans leo Alhamisi (Agosti 19) kitakamilika kwa asilimia 100, kwa kutimiza idadi maalum ya wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Ukamilifu wa kikosi cha klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, utatimia baada ya kuwasili kwa, beki kutoka nchini DR Congo Yanick Bangala Litombo mjini Marrakech, Morocco.

Beki huyo aliyemalizana na Uongozi klabu hiyo mwishoni mwa juma lililopita, amesema anatarajia kuwasili mjini humo mishale ya saa tatu usiku.

“Nitafika huko Morocco leo, nilikuwa huko ila niliomba muda niende nyumbani mara moja na viongozi wakanikubalia, sasa niko tayari kuanza maisha mapya na Yanga, nakuja.” amesema staa huyo ambaye ni mbadala wa Lamine Moro.

Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa Young Africans kwa ajili ya msimu mpya 2021/22 ni Djigui Diarra, Erick Johora, Djuma Shaban, Jesus Muloko, David Bryson, Dickson Ambundo, Khalid Aucho, Heritier Makambo na Fiston Mayele.

R Kelly kutiwa kifungoni
Taliban wamewasihi watu kuondaka uwanja wa ndege