Bao la Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Pappe Ousmane Sakho alilolifunga dhidi ya ya RS Berkane ya Morroco limeingia kwenye orodha ya mabao bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika yaliyofugwa mwishoni mwa juma lililopita.

Sakho ambaye ni Raia wa Senegal aliifungia Simba SC bao hilo pekee na la ushindi kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Jumapili (Machi 13).

Awali kiungo huyo aliifungia Simba SC bao katika ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na bao lake likatangazwa kuwa bao Bora katika mzunguuko wa kwanza wa Michuano ya Afrika kwa vilabu.

Hii ni mara ya pili kwa Sakho kung’araa katika viwango vya ubora wa Shirikisho la soka Barani Afrika kupitia kipengele cha kufunga mabao bora.

Mabao mengine yaliyoingia kwenye orodha ya mabao bora kwa mzunguuko wa nne katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ni bao lililofungwa na Hassan Ally wa Al Masry.

Katika mchezo huo Al Masry iliyokua nyumbani katika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS otoho ya Congo Brazaville

Bao lingine lililoingia katika mabao bora ya Kombe la Shirikisho Mzunguuko wanne ni la Walid El Karti wa Pyramid FC ya Misri.

Wakicheza katika Uwanja wa ugenini wa Hammadi Agrebi mjini Tunis-Tunisia, Pyramid walilazimisha matokeo ya sare ya 1-1.

Bao la Mutez Husayn wa Al Ahly Tripoli nalo limeingia kwenye orodha ya mabao bora yaliyofungwa katika mzunguuko wanne wa Kombe la Shirikisho.

Al Ahly Tripoli walikua ugenini mjini Lusaka wakicheza dhidi ya Zanaco FC ya Zambia iliyokubali kibano cha 3-2
Orlando Pirates ya Afrika kusini nayo imeingiza bao bora katika orodha hiyo, lililofungwa na Fortune Makaringe kwenye mchezo dhidi ya Royal Leopards ya Eswatini iliyokubali kulala kwa mabao 3-0.

Habari Picha: Makamu wa Rais afungua daraja la magara
TBS yatoa semina kwa wadau sekta ya dawa na vifaa tiba