Kwa mujibu wa Ripoti mpya inasema kuwa Afrika inahitaji kuwekeza kiasi cha dola bilioni 50 kwa mwaka ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

Umoja wa Afrika na taasisi ya hali ya hewa duniani umeonya kuwa watu maskini wapatao milioni 120 wanakabiliana na mafuriko, ukame, kuhama makazi yao na joto lililopita kiasi ifikapo mwishoni mwa muongo kama hakuna jitihada zitafanyika.

Ripoti imeonya kwamba “Kupungua kwa kasi kwa barafu za mwisho zilizobaki mashariki mwa Afrika, ambazo zinatarajiwa kuyeyuka kabisa katika siku za usoni, kunaashiria tishio la mabadiliko ya tabianchi yasiyoweza kurekebishwa kwa mfumo wa dunia”. 

Milima mitatu tu barani Afrika imefunikwa na barafu ambayo ni mlima Kenya, Mlima Rwenzori nchini Uganda, na Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Ingawa barafu ni ndogo sana kuweza kuchukua nafasi ya hifadhi kubwa za maji, WMO ilisisitiza umuhimu wake katika utalii na kisayansi. 

Hivi sasa, viwango vya kupungua kwa barafu hiyo ni vya juu kuliko wastani wa kimataifa na kutoweka kabisa kwa barafu kunawezekana ifikapo miaka ya 2040. 

Afrika imepata joto haraka kuliko wastani wa ulimwengu ingawa imewajibika kwa 4% tu licha ya uzalishaji wa hewa chafu duniani.

Siku ya lishe kitaifa kufanyika Tabora
Mwanafunzi wakitanzania auawa Marekani