January 17 2017 kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wa mwanamziki wa Bongo fleva Barakah the prince amewathibitishia mashabiki wake kwamba yuko karibuni kupata mtoto na mpenzi wake wa muda mrefu Naj.

Kupitia mtandao huo Barakah ameandika ” Tumeumbwa kuijaza dunia na hawa ma singa singa nakungoja mwana kwa ham” akamalizia kwa kumtag mpenzi wake huyo Naj.

Ambapo Naj kwa wakati wake alipata nafasi ya kujibu mtandaoni alichokituma Baraka the Prince  na kuandika ”Calm down guys am not preganat sema tu nilikula chapati nyingi na kachori”. (Tulieni jamani sina mimba sema tu nilikula chapati nyingi na kachori ).

Baraka na Naj walitafutwa kwa mahojianao na baadhi ya vyombo vya habari, kuhusu ukweli wa jambo hilo, ambapo Naj alisema kila kitu kinaenda kwa mipango hivyo hakuwa  tayari kuzungumzia jambo hilo ila kuahidi mashabiki wa Baraka the Prince na Naj, wakati  ukifika wataweka wazi jambo hili alidai sio vizuri kwa sasa kulizungumzia.

Lakini pia Naj alipata nafasi ya kueleza matamanio yake kuhusiana na jinsia ya mtoto wake wa kwanza, na kueleza kuwa anatamani sana kupata mtoto wa kike.

”Unajua mimi ndugu zangu wengi wanawatoto wachanga kwa hiyo nimeona na najua mvulana akiwa anakuwa inakuwaje na msichana akiwa nakuja inakuwaje, ‘so i need a girl’ ”.

Alimalizia kwa kusema ” Unajua mtoto wa kike unaweza fanya nae vitu vingi sana hasa hasa kwa mimi kama mama”.

 

Video: Maiti iliyozikwa Mbeya yakutwa nyumbani, Mbowe ataja kinachowaliza
NEC yawataka wasimamizi kuzingatia maadili ya uchaguzi