Aliyekuwa mwanafamilia wa lebo ya RockStar4000, Barakah Da Prince ameeleza sababu za kuitosa lebo hiyo hivi karibuni.

Baraka aliweka wazi uamuzi wake wa kujiondoa RockStar4000 siku chache baada ya lebo hiyo kumtangaza Ali Kiba kuwa Mkurugenzi wake mpya ambaye aliingia kwa kasi ya kumsajili Ommy Dimpoz.

Mkali huyo wa ‘Nisamehe’ amesema kuwa kulikuwa na  mambo mengi yaliyosababisha kuchukua hatua hiyo ikiwa ni pamoja na kucheleweshwa kwa mikakati ya kazi zake.

“Walichotaka kukifanya kwangu kinamanufaa kwa sababu target yao kwangu ni manufaa. Wameplay part yao,” Barakah amefunguka alipohojiwa na Ayo TV.

“Ukiona mtu imefika hatua… hata kama ana uwezo wa kufanya lakini kinafanywa kwa kuchelewa wakati kinakuondoa katika utaratibu wako au mikakati yako ya kikazi, hauna budi kufanya maamuzi magumu kwa faida yako,” aliongeza

Hata hivyo, amesema kuwa kuna vitu ambavyo Rockstar4000 wamemfanyia ambavyo vitabaki kwenye historia yake na kwamba hatasau walivyomsaidia kupiga hatua nyingine.

Katika hatua nyingine, mwimbaji huyo amewageukia mashabiki wake akiwataka kutumia muda mwingi kufuatilia muziki wake na sio uamuzi wake kwenye masuala yake binafsi.

“Wewe kama shabiki deal na muziki wangu tu. Personal life (maisha binafsi) na personal business yangu wewe haikuhusu. Na sometimes hupaswi kuangalia nani anasema nini na anafanya nini kuhusu wewe, fanya kile ambacho unaamini ni maamuzi sahihi yenye faida kwenye maisha yako,” amefunguka.

Alisema hivi sasa anaendelea na mipango yake na kwamba anatarajia kuachia albam yake mwaka huu ambayo itasimamiwa na Bana Music. Alisisitiza kuwa hivi sasa yeye ndiye atakayeusimamia muziki wake na hayuko chini ya mtu yoyote isipokuwa wanafanya biashara tu.

Afanyiwa upasuaji wa ubongo akiwa anapiga gitaa
JPM: Tumekaribisha mazungumzo na kama wakichelewa, nitafunga migodi yote