Wachezaji na makocha wa klabu za Ligi Kuu ya England hawatalazimishwa kuvaa barakoa kwenye viwanjani wakati Ligi hiyo itakaporejea Juni 17.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa huku juma moja likisalia kabla ya kurudi kwa ligi ya England (EPL). Licha ya kutolazimika kuvaa barakoa lakini wachezaji na makocha wameaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya virusi vya Corona kama kutokaribiana baada ya goli kufungwa.

Hakutakuwa na watoto waokota mipira, na mfumo wa kupulizia dawa mipira utaendelea kutumika wakati, mchezo ukiendelea.

Mtanange wa kwanza utakuwa wa Aston Villa dhidi ya Sheffield United Juni 17. Chama cha Soka England (FA) juma lililopita kilisema kutakuwa na dakika moja ya kuwakumbuka walipoteza maisha kutokana na janga la virusi vya Corona.

Hata hivyo, bado idadi ya watu kuingia viwanjani itabaki pale pale 300 ambapo watu 110 watawahusisha wachezaji, makocha, na waamuzi watakuwa eneo la kuchezea na wanaobaki watakaa majukwaani.

Ushahidi: Waziri Mkuu msaafu alivyolipa majambazi kumuua mkewe kisa mchepuko
CCM yatangaza siku 15 za mchuano kumpata mgombea urais 2020