Baraza la kijeshi linaloongoza nchi ya Sudan linakutana na waandamanaji kujadilia kipindi cha mpito wa kisiasa baada ya mazungumzo hayo kusitishwa kwa siku tatu huku barabara zikisafishwa nje ya eneo kuu walikokusanyika waandamanaji katika mji mkuu wa Khartoum.

Pande hizo mbili zimeshiriki duru kadhaa za mazungumzo tangu jeshi la nchi hiyo lilipoipindua serikali ya Rais, Omar al-Bashir mwezi uliopita baada ya miezi minne ya maandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

Aidha, naibu mkuu wa baraza hilo la kijeshi Jenerali, Mohammed Hamdan Dagalo amesema kuwa maafisa usalama wamewakamata wahusika wa mashambulizi dhidi ya waandamanaji wiki iliyopita yaliosababisha vifo vya watu watano ikiwa ni pamoja na afisa mmoja wa kijeshi.

Wanajeshi na waandamanaji hao wamesema kuwa mashambulizi hayo yalitekelezwa na wafuasi wa al- Bashir. wakati huo huo Saudi Arabia imefahamisha kuwa imeweka dola milioni 250 kwenye benki kuu ya Sudan, kuimarisha hali ya kifedha ya nchi hiyo na kuipunguzia shinikizo sarafu ya pauni ya Sudan.

Hata hivyo, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zilitoa msaada wa dola bilioni 3 kwa nchi hiyo baada ya kuondolewa kwa Rais Bashir.

 

Video: Wanaonyatia Urais CCM 2020 wakemewa, Viongozi wa kanisa katika tuhuma nzito
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 20/2019