Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara samba sc hatimae wamemtangaza CEO wao mpya Barbara Gonzalez anaechukua nafasi ya Senzo Mazingizo Mbatha

Barbara Gonzalez amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi mtendaji   wa taasisi ya  Mo Dewji Foundation, taasisi iliyoanzishwa na bilionea mdogo zaidi barani afrika , Mohammed Dewji.

Barbara ameshiriki majukumu ya kuendesha mipango ya maendeleo katika taasisi hiyo ya kitanzania .

Pia Gonzalez amekuwa akihudumu kama mshauri wa bodi ya Young African Leaders Initiative (YALI) ,pamoja na jumuhia ya uongozi afrika mashariki na kati .

 YALI ilizinduliwa na aliekuwa raisi wa marekani  Barack Obama kama ishara ya kusukuma gurudumu la kizazi kipya kwenye uongozi wa afrika  

Awali, Gonzalez alikuwa mshauri wa taasisi ya  Deloitte Consulting Limited Tanzania. alijihusisha na miradi ya mbalimbali ya jamii pamoja na ile ya  USAID, UNICEF, benki ya dunia  na  Plan International.

Gonzalez ni muhitimu  wa shahada ya uzamili ya usimamizi wa maendeleo toka  chuo cha uchumi na siasa  London.

Pamoja na digrii ya shahada katika uchumi na siasa kutoka chuo cha Manhattanville College in Purchase, New York.

Rungwe :Nitaendesha serikali yenye haki kwa kila mtu
India, China kumaliza mvutano