Afisa mtendaji Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara ‘CEO’ Simba SC Barbara Gonzalez amefurahishwa na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly na kusema unawapa nguvu ya kuendelea kupambana zaidi.

Barbara alithibitisha furaha yake alipozungumza na Dar24 Media mara baada ya mchezo huo kumalizika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na kushuhudia Simba SC ikifikisha alama sita na kuongoza msimamo wa Kundi A.

“Vijana wetu wamepambana kuhakikisha wanaliwakilisha vyema  Taifa la Tanzania kuonyesha soka letu nilaushindani na tumeamua kupambana,”

“Kazi ndio imeanza mashabiki waendelee kuishangilia timu yao, ili mwaka huu tufanye vitu vyakushangaza.” amesema Barbara

Wakati Barbara anatoka uwanjani hapo kwenda kupanda gari yake, alisindikizwa na msafara wa wanaume wasiopungua 10 huku akipita katikati yao.

Baada ya kuona hivyo mashabiki walianza kumshangilia na kumuita ni mwanamke wa shoka.

Wakati SImba SC ikiifunga Al Ahly, AS Vita Club nayo ilipata ushindi ugenini nchini Sudan kwa kuwafunga wenyeji wao  Al Mereikh mabao 1-4.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaongoza msimamo wa ‘KUNDI A’ ikiwa na alama sita, ikifuatiwa na AS Vita Club yenye alama tatu sawa na Al Ahly wanaoshika nafasi ya tatu, lakini wanatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Al Mereikh inaburuza mkia wa kundi hilo kwa kutokua na alama yoyote huku ikipoteza michezo yake dhidi ya Al Ahly pamoja na AS Vita Club.  

Kaze afichua siri nzito Young Africans
TFF yatangaza vituo Ligi ya Mabingwa 'RCL'