Afisa Mtendaji Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Barbara Gonzalez kwa mara ya kwanza amekutana na aliyekuwa kocha Mnyama Sven Vandebroek.

Wawili hao wamekutana nchini Morocco, kufuatia uwepo wa Barbara nchini humo kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya kikosi cha Simba SC kuelekea msimu ujao.

Barbara alifanya kazi na kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji, kabla ya kuondoka Simba SC mwishoni mwa mwaka 2020, akiiacha ikiwa imetinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuzifunga Plateau United ya Nigeria na FC Platnums ya Zimbabwe.

Sven kwa sasa ni kocha wa klabu ya FAR Rabat ya Morroco.

Young Africans yatupwa nje Kagame Cup
Jarida la wananwake suluhu ya kutatua changamoto