Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza amejibu lawama zilizotolewa na msanii Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz akidai kuwa Basata haikufuata utaratibu pindi wanazifungia nyimbo 15 za wasanii wa bongo fleva.

Lawama hizo ni kufuatia wasanii kufungiwa nyimbo zao bila kupewa barua yenye maelezo ya kuzifunga.

Mungereza amesema si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosea kama ambavyo Diamond ameeleza, na kudai kuwa kitendo cha Diamond kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ni kama ameitukana Serikali jambo ambalo katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.

Aidha amesema amesikitishwa na kauli za Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyoelezwa na Waziri Shonza.

Katika malalamiko yake, Daimond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.

Jana Waziri Shonza amesema hawezi kujibizana na Diamond Platinumz kwa sababu alichokifanya si maamuzi yake binafsi na kwamba anaona ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.

 

Rais wa Myanmar ajiuzulu
Video: Sisi hatutekelezi Ilani ya CCM, Polepole anahaha tu- Meya Ubungo

Comments

comments