Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limeufungia rasmi wimbo mwingine wa Nay wa Mitego aliouachia hivi karibuni, ‘Pale Kati Patamu’.

Msemaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amemtaja Nay wa Mitego kama msanii ambaye amekuwa akitumia lugha za matusi na zenye kudhalilisha wanawake kwenye nyimbo zake kinyume na maadili.

Amesema kuwa Baraza hilo lilishashamuita na kumkanya Nay wa Mitego ambaye aliahidi kuachana na tabia ya kutoa nyimbo za aina hiyo lakini amerudia tena.

“Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine,” amesema Mngereza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Pale Kati

“Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama,” aliongeza.

Huu ni wimbo wa pili wa Nay wa Mitego kufungiwa mwaka huu baada ya kuipiga tofali ‘Shika Adabu Yako’.

Waziri Mkuu Afungua Duka la MSD Ruangwa, Kuhudumia Hospital 524
Trump: Ningetangaza Vita ya Dunia baada ya Shambulizi la Ufaransa