Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wasanii wa muziki nchini kuwa makini pindi wanapotaka kuingia makubaliano ya kikazi (mikataba) ili waweze kuepuka migogoro isiyokuwa na tija.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza baada ya kuwepo kwa malalamiko mbalimbali kutoka kwa wasanii, wakidai wanadhulumiwa na wasimamizi wa kazi zao ‘Manager’ kutokana na mikataba waliyokuwa wameingia bila ya kuipitia kwa umakini.

“Wasanii msiingie mikataba yoyote bila ya kupata ushauri wa kisheria ambapo ushauri huo unatolewa Baraza pamoja na taasisi nyingine za kisheria ikiwemo hata Wizara ya Habari katika suala zima la mikataba. Changamoto hii ipo lakini muda mwingine wasanii wenyewe inawezekana wakawa ndio chanzo cha migogoro hiyo,”amesema Mngereza

Hata hivyo, Mngereza amedai kuwa wao kama BASATA hawana vigezo vyovyote walivyoviweka kwa watu wanaotaka kusimamia kazi za wasanii, kwa madai jambo hilo limekuwa likifanywa kibinafsi baina ya msanii na mtu fulani kulingana na matakwa yao.

Jeshi la Polisi laomba msamaha
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 22, 2018