Mbunge wa Nzega Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe, amemtakia heri waziri mpya wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa huku akibainisha kuwa utendaji kazi wake si wa mashaka.

Amemwelezea Bashungwa kama mtendaji ambaye uwezo wake wa kutekeleza majukumu yake, bila shaka atafikia matarajio ya taifa kwenye wizara hiyo.

”Hongera sana Innocent, nakutakia heri kwa tunaokufahamu tunaamini utafikia matarajio ya wengi na taifa ,Kila la kheri Chief.”, amesema Bashe.

Aidha, Bashungwa ambaye ni Mbunge wa Karagwe aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, aliwahi kuwa Naibu waziri wa Kilimo akiteuliwa na Rais Magufuli, Novemba 10, 2018.

Katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Bashungwa amechukua nafasi ya aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Joseph George Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Juni 8, 2018.

 

Aliyekuwa RPC akutwa amekufa nje ya nyumba yake
Video: TRA kaa la moto, Sababu tisa zang'oa mawaziri 15

Comments

comments