Wakati joto la uchaguzi mdogo wa majimbo ya Ukonga na Monduli likizidi kupanda, Mbunge wa Nzega Mjini kwa tiketi ya CCM, Hussein Bashe amewataka wananchi kupuuzia hoja zinazotolewa na makada wa Chadema kukosoa uamuzi wa Mwita Waitara kukihama chama hicho.

Bashe ambaye alikuwa mmoja kati ya waliomuunga mkono Edward Lowassa alipotangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea urais akiwa CCM mwaka 2015, akiwa kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi Waitara alisema kuwa suala la mwanasiasa kuhama chama chake anapoona hakina tija ni suala la kawaida na kwamba hata yeye angefanya hivyo endapo CCM itakosa tija kwa wananchi.

“Hakuna jambo linalonisikitisha mimi kama kijana, eti kwamba mwanasiasa anapohama chama anatuhumiwa kuwa amenunuliwa. Hata sisi wana CCM chama chetu kinaposhindwa kusimamia maslahi au kutatua matatitzo ya wananchi, ukiona mimi nimebaki CCM jua tunalinda matumbo yetu,” anakaririwa na Mwananchi.

Mwanasiasa huyo machachari alitoa mifano wa wanasiasa ambao waliwahi kuihama CCM na kuelekea upinzania akiwemo Augustino Mrema, Maalim Seif Sharif Hamad na hata aliyekuwa waziri mkuu na mtu aliyemuunga mkono, Edward Lowassa na kueleza kuwa wakati huo CCM hawakusema kuwa wamenunuliwa.

“Wanaosema tumemnunua Waitara wao watuambie walimnunua kwa shilingi ngapi mwaka 2008?” alihoji Bashe, akirejea uamuzi wa Waitara aliyekuwa kiongozi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuhamia Chadema mwaka 2008.

Waitara alikuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema tangu mwaka 2015, lakini alijiuzulu mwaka huu na kuhamia CCM ambapo amepewa nafasi ya kugombea tena nafasi hiyo.

Msanii aomba aendelee kufungwa kwa kujaribu kumuua Rais Kagame
DC Kasesela azidi kuineemesha Iringa, agawa hati za ardhi zaidi ya vijiji 33