Waziri wa kilimo Hussein Bashe amezindua rasmi usajili kwaajili ya washiriki wa kongamano la usalama wa chakula litakalofanyika septemba4, hadi 5 mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri Bashe amesema kongamano hilo litaangazia nafasi ya Bara la Afrika katika matumizi ya mbinu bunifu zitakazohakikisha Dunia inakuwa na usalama wa chakula.

“Wakati tukiendelea na jitihada za kuliwezesha Bara la Afrika kuwa kitovu cha usalama wa chakula Duniani, tunapaswa kuwapa kipaumbele vijana na wanawake katika harakati hizi’ amesema Bashe.

Waziri wa kilimo Hussein Bashe

Aidha amesisitiza umuhimu na nafasi ya viongozi wa Afrika katika kuchangia uwepo wa usalama wa chakula ngazi za Taifa na Bara huku akisisitizia ushiriki kwa vijana na wanawake.

Hata hivyo Bashe amesema kuwa mkutano wa AGRF mwaka huu utafungua milango ya matumizi ya ubunifu katika kuimarisha Kilimo pamoja na kufungua milango ya uwekezaji zaidi itakayohakikisha uwepo wa ubunifu, utugwaji wa sera Bora pamoja na uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa jukwaa hilo Amath Pathe Sene amesemae kuwa ubunifu, Sera bora, uwekezaji wa kimkakati ni njia sahihi katika kuhakikisha upatikanaji wa mifumo imara ya chakula.

“AGRF 2023 itahusisha programu mbalimbali Kati ya wadau ambapo watapata wasaha wa kujadiliana na kubadilishana uzoefu” – amesema Amath.

Mkurugenzi huyo pia amesema septemba 3,2023 wagenj wa mkutano watapata wasaha wa kutembelea na kijionea shughuli za kilimo zinazofanywa na watanzania na kujioneae mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 15, 2023
Aliyedaiwa kujiteka akamatwa