Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amesema kuwa mfumo wa kodi nchini umesababisha gharama za uzalishaji bidhaa kuongezeka na kudumaza mazingira rafiki ya uwekezaji.

Amesema kuwa kuwa licha ya mwaka 2016 kumwambia Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuwa anasubiri aone miujiza katika wizara hiyo, hadi sasa inashangaza kuona hakuna kilichotokea.

Aidha, mbunge huyo ameitaka Wizara hiyo, kukutana na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji yatakayomsaidia Rais Dkt. John Magufuli kutimiza ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

“Muujiza wa kwanza ulikuwa ni kuona namna gani Wizara ya Viwanda inaweza kuunganisha mambo matatu ambayo amekabidhiwa. Rais aliamua kwa makusudi kuunganisha biashara, viwanda na uwekezaji ili kufikia lengo la mapinduzi ya viwanda, lakini hadi leo tunazungumzia General Tyre, Liganga na Mchuchuma. Kuna matatizo ya msingi ya biashara lakini huoni kwenye mpango wetu namna ya kuyashughlikia,”amesema Bashe

Hata hivyo, ameongeza kuwa licha ya Mwijage kutaja vipaumbele vya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19, hakuna mpango unaoonesha kuondoa matatizo yaliyopo kwenye mifumo ya kodi, miongozo na sheria katika kufanya biashara nchini.

 

Serikali yataifisha Migodi ya Madini nchini
Magazeti ya Tanzania leo Mei 12, 2018