Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ambae pia ni Mbunge wa Karagwe amefanya ziara jimboni hapo ikiwa na lengo la kuzungumza na wananchi pia kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo kwa kuleta maendeleo chanya.

Aidha baadhi ya changamoto katika jimbo hilo ni pamoja na Miundo mbinu ya barabara, maji, ardhi, elimu, afya pamoja na kero za kukosa umeme katika baadhi ya kata, huku akiwasihi wananchi kuwa vumilivu na kusubiri mradi wa maji wa Rwakanjunju ambao utauwa suluhu wa changamoto ya maji katika jimbo hilo.

“Miradi hii midogomidogo ya maji ni kama panadol lakini baba lao ni mradi mkubwa wa Rwakajunju ambao utakua ni mwarobaini wa kuondoa changamoto ya maji karagwe kwani vijiji zaidi ya 30 vitanufaika,” Amesema Waziri Bashungwa.

Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amewahasa Maafisa Michezo katika kila Kata na Wilaya kutunza viwanja vya michezo mashuleni walivyonavyo lakini pia kama shule haina kiwanja wafanye mpango wa kuwa na kiwanja cha machezo.

“Mashule lazima yawe na viwanja vya michezo ondoeni fikra kwamba mtoto lazima akae madarasani bila michezo tutoe, Napenda watoto wetu waendeleze vipawa vyao vya michezo ni ajira tosha” amesema Mhe. Bashungwa

Sambamba na hayo yote Waziri Bashungwa pia amekutana na Madiwani wote wa kata za jimboni Karagwe kwa maendeleo ya jimbo.

Mradi chujio la maji kukamilika September 2021
Mwana FA: Coastal Union haishuki daraja