Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa ameitaka Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi kuunga mkono mapambano ya adui ujinga yanayofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kila Mtoto aliyefikisha umri kuanza Shule apelekwe kuanza masomo.

Bashungwa ameyasema hayo mwishoni mwa wiki na kuongeza kuwa, jukumu kubwa la Jumuiya ya Wazazi ya CCM ni kuhamasisha na kuendeleza elimu nchini ili kufuta adui ujinga na kusimamia maadili katika jamii.

Amesema, Serikali imeweka Mkazo mkubwa katika kuboresha utoaji elimu nchini ambapo imejenga shule za msingi kila Kijiji na Shule za Sekondari kila kata nchi nzima. 

Aidha, amesema katika utawala wa miaka miwili ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha ujenzi wa miundombinu ya shule shikizi zaidi ya 3,000 na ujenzi wa madarasa zaidi ya 20,000 kwa awamu mbili.

Amesema pamoja na Juhudi za  Serikali kuwezesha utoaji wa elimu bure kunzia darasa la awali mpaka kidato cha sita, lakini takwimu zinaonesha wanafunzi walioandikishwa na walioanza masomo bado ni wachache.

Hata hivyo, ametoa wito kwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi kuishi misingi ya kuasisiwa kwa Jumuiya hiyo, na kuondokana na hali ya unyonge ikiwa ni pamoja kusimamia elimu na maadili ya vijana, katika Jamii yetu.

Tahadhari ya shambulizi: Serikali yaikosoa taarifa ya KLM
Majaliwa asisitiza michezo, majukumu ya kazi