Basi la Mwendokasi, jana lilimgonga mtu mmoja mlemavu na kusababisha kifo chake papohapo katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya, ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili usiku katika makutano ya barabara ya Msimbazi na Uhuru.

Alisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa dereva katika eneo hilo lenye mataa ya kuongoza magari, mwendo ambao haukutegemewa katika eneo hilo. Alisema kuwa mwili wa marehemu uliharibika vipandevipande kutokana na ajali hiyo.

Tangu kuanzishwa kwa usafiri huo uliopunguza adha ya usafiri jijini humo, ajali kadhaa zimeripotiwa ikiwa ni pamoja na mabasi hayo ya mwendo kasi kugongana na bodaboda au kugongana na magari ya watu binafsi pamoja na daladala. Watu kadhaa wameripotiwa kufariki kutokana na ajali hizo ikiwa ni pamoja na mtoto mdogo aliyekuwa amebebwa na mama yake kwenye bodaboda.

Ndani ya kipindi cha siku 20 tangu yalipoanza kutoa huduma, mabasi 34 yaliripotiwa kupata ajali kwa nyakati tofauti.

Chadema Waifikisha Serikali Mahakama kuu
Habari Mpasuko: Magufuli afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri