Watu wanne wanashikiliwa na polisi mara baada ya kumvamia mwanaume mmoja akiwa nyumbani kwake kwa kutumia silaha bandia aina ya bastola za kuchezea watoto.

Ofisa wa polisi Nigeria, Lagos, Chike Oti ambaye ni msemaji amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wanne waliofanya tukio hilo .

Mvamiwa alipata nafasi ya kuongea na kusema kuwa majambazi hao walivamia nyumbani kwake na kumtishia kumuua kwa kutumia bastola hizo na silaha nyingine za ncha kali walizokuwanazo.

Hata hivyo kabla majambazi hao kuanza kutekeleza azimio lao la uporaji wa mali, jopo la polisi lilivamia eneo hilo na kuwakamata watuhumiwa hao waliovamia eneo hilo wakiwa na begi lenye silaha feki mbili aina ya bastola za kuchezea watoto huku wakiwa na kisu pamoja na gundi kubwa aina ya cellotape.

Watuhumiwa walifahamika kwa majina ya Azeez Bankole (20), Israel Okoye (20), Timitauyo Ogundayo (19) na Abeeb Bamghopa (22) ambao walitiwa mbaroni wakiwa katika eneo la tukio.

Hata hivyo kesi hiyo tayari ipo mahakamani na upepelezi wa kina ukiwa unaendelea kufanywa na vyombo husika

Davido, Chioma ndoa yaiva
R Kelly apanga kukimbilia Afrika, wanaodai aliwabaka wacharuka

Comments

comments