Wachezaji wa Singida Big Stars, Shafiq Batambuze na Yusuf Kagoma hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachoikabili Ruvu Shooting baadae leo Jumanne (Juni 06) kwenye Uwanja wa Liti, mkoani Singida kutokana na kuwa idadi kubwa ya kadi za njano.

Singida imepanda daraja msimu huu na inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 51 katika michezo 28 iliyocheza na itamaliza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Namungo FC Juni 9 mwaka huu katika Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi.

Msemaji wa timu hiyo, Hussein Massanza amesema ni pengo kuwakosa wachezaji hao lakini benchi la ufundi limejipanga kuhakikisha nafasi zao zinazibwa.

Katika hatua nyingine, SBS imepanga kuitumia mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting kuwaaga mashabiki kwa kujitoa kwa ajili ya klabu hiyo.

“Utakuwa mchezo wetu wa mwisho nyumbani tunafikiria kuweka mashabiki waweze kuangalia bure pasiwe na kiingilio. Nimejaribu kuzungumza na wachezaji na benchi la ufundi wamesema wanajiandaa kutoa burudani,” amesema Massanza na kuongeza;

“Niwaambie mashabiki waanze kujiandaa wenye jezi waziweke vizuri napengine patakuwa na saprize kikubwa atakayekuwa na jezi atafaidika na hiyo sapraizi.

Bruce Kangwa aigawa Azam FC
Felix Sunzu awapa ujanja viongozi Simba SC