Mshambuliaji wa Chelsea aliyeelekea katika klabu ya Borussia Dortmund kwa mkopo, Michy Batshuayi amefunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza na klabu yake mpya dhidi ya Cologne.

Batshuayi, ambaye ameelekea Dortmund hadi mwisho wa msimu huu alifunga bao lake la kwanza katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza bao la pili baada ya saa moja.

Aidha, bao jingine lilifungwa na Simon Ziller kabla ya Jorge Mere kuwasawazishia wenyeji wa mchezo huo ambao walikuwa wameukamia.

Hata hivyo, Ushindi huo unaipeleka Dortmund hadi nafasi ya pili katika ligi kuu ya Ujerumani maarufu kwa jina Bundesliga.

China yaionya Marekani
Serikali kuimarisha masoko ya mazao