Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum Bausi ndoto zake zipo pale pale za kuwa Rais wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) ambapo leo hii baada ya kamati ya uchaguzi wa ZFA kutangaza tarehe ya uchaguzi Bausi amesema nia yake ipo pale pale na atagombania nafasi ya Urais wa ZFA.

Akizungumza nasi Bausi amesema ana lengo la kubadilisha soka la Zanzibar ambapo yeye atagombania nafasi ya Urais na atatangaza siku ambayo atakayokwenda kuchukua fomu ya kugombania.

“ Nia yangu ipo pale pale na nimefurahi kuona kuchukua fomu shs laki mbili tu, kwasababu mwanzo tulisikia laki tano, nia yangu na dhamira yangu ipo pale pale na naamini ntalikomboa soka la Zanzibar nikiwa kama Rais wa ZFA, mimi ni mtu pekee naweza kuliokoa Jahazi la hili ambalo linazama”. Alisema Bausi.

Katika uchaguzi wa mwaka 2012 Kocha Salum Bausi alichukua fomu ya kugombania nafasi hiyo lakini aliishia njiani mwishoni ambapo wadau wengi wa soka bado wanahofu kubwa sana kuchukua fomu za kugombania nafasi hizo 3 za juu kwenye chama hicho ambapo wakiamini hata wakigombania hawatoshinda nafasi yoyote kutokana na viongozi waliokuwepo Madarakani ni vigumu sana kuwang’oa.

Misri Kuwakabili Serengeti Boys Juma Lijalo
Rage Aishauri TFF Kudai Fidia Za Mchezo Dhidi Ya Chad