Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA, (Bavicha), Patric Ole Sosopi, amesema kuwa kuna lengo la kukifuta Chama hicho kwani nguvu inayotumika kuumiza upinzani hususani CHADEMA ni kubwa sana.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kuna watu wanaotumwa  kuichafua CHADEMA kwa ajili ya kutafuta sababu ya kukifuta chama hicho.

“Tumewapuuza kwa muda mrefu, tukiamini vyombo husika vitachukua hatua dhidi yake lakini kwa kuwa wanamtuma anaendelea kuwa salama.  Hila za kuifuta CHADEMA hazitafanikiwa. Kama tulianza na madiwani 3 leo kina zaid ya madiwani 70 hakitaweza kufutwa kwa njia yoyote,”amesema Sosopi

Amesema kuwa Chadema inawahakikishia Watanzania kuwa jitihada za kuifuta CHADEMA hazitafanikiwa na hakuna mtu atakayeifuta CHADEMA.

Hata hivyo, Sosopi amesema kuwa vijana wa CHADEMA wapo tayari kulaumiwa baadaye lakini siyo kuacha chama hicho kiweze kufutwa na kusisitiza kwamba vijana wa chama hicho wako imara na hawaogopi kufa.

Joshua ampiga Parker, amnyooshea ngumi Wilder
Ngorongoro Heroes yajiweka njia panda