Baraza la Vijana Chadema leo limekutana jijini dare es salaam kujadiliana juu ya kuweza kudhibiti mikutano ya kisiasa ambayo imekatazwa na jeshi la polisi pamoja na Rais wa Tanzania Mh. John Magufuli.

Akizungumza leo katika kikao cha kamati ya maadili  Mwenyekiti wa Bavicha Patrobas Katambi amesema baada ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwazuia kwenda dodoma kwa ajili ya kufanya kile walichokiita kusaidia jeshi la polisi kikao wanachojadili leo kitatoka na majibu ya nini kifanyike.

”Kikao hiki kitatoa majibu yote na tutasema hapo kesho baada ya muafaka kupatikana, Baada ya Mwenyekiti Mbowe kuzuia sasa tunajadiliana na hata tukienda hatuwezi kufanya fujo kama wanavyodhani, ni hofu zao”.- katambi

Patrobas amesema wapo viongozi wengi wa Ccm ambao wanafanya mikutano wakitumia kivuli cha Serikali jambo ambalo vyama vya upinzani wakifanya wanaonekana kuipinga serikali.

”Agizo la IGP pamoja na Mh Rais Magufuli limeonekana kuwa tatizo kwani wahanga wakubwa wa kauli ya kutofanya mikutano mpaka 2020 wamekuwa chadema na Act”. alisema Katambi.

Aidha ameongeza kuwa CCM kufanya mkutano tar 23 ni ukiukwaji wa misingi ya demokrasia nchini kwani wapo wananchi wengi wamedhulumiwa haki ya kuwasikia viongozi wao katika majukwaa kwa kile kilichoitwa kufanya siasa.

”IGP pamoja na Rais wameshindwa kusimamia kauli zao kwa za kuzuia mikuutano ya kisiasa mpaka 2020,  na hofu kubwa ya kuweka ulinzi dodoma ni hofu kwa kuwa wamedhulumu haki z wengi” -Katambi.

Katika Ufunguzi wa kikao hiko aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia umoja vyama vinavyounda Ukawa Mh. Edward Lowassa aliwashauri Bavicha na kuwaambia waache wananchi wawahukumu kwani Mwenyekiti atakayechaguliwa atapelekwa uwanjani na utakuwa ni mkutano wa hadhara.

”Mpaka sasa tayari ujumbe umewafikia, mmefanya vizuri lakini ningewashauri waacheni wajihukumu kwa wananchi kwa kauli zao, ninavyojua Mwenyekiti atapelekwa Stadium na utakuwa ni mkutano hivyo wanajihukumu peke yao”. – Lowassa

Ccm wanatarajia kufanya mkutano mkuu maalum wa kumkabidhi Rais John Magufuli madaraka  ya Uenyekiti wa chama hicho mwisho wa wiki hii julai 23

 

 

Lowassa: Bavicha Twendeni Vijijini
Tanzania Yapata Tuzo Mkutano AU