Wakati mipango wa uhamisho wa kiungo kutoka nchini Armenia, Henrikh Mkhitaryan ambaye huenda akacheza soka lake nchini England msimu ujao ikiendelea, uongozi wa klabu ya Borussia Dortmund umekwama katika mipango ya kutaka kuziba pengo litakaloachwa na mchezaji huyo.

Mkhitaryan ameripotiwa kuwa katika hatua za mwisho kujiunga na Man Utd, baada ya ada yake ya usajili kukubaliwa na klabu hiyo, ambayo kuanzia msimu ujao wa ligi itakua chini ya meneja kutoka nchini Ureno, Jose Mourinho.

Tayari Borussia Dortmund, wameshajipanga kumsaka mbadala wa Mkhitaryan kwa kumtupia jicho kiungo wa Ujerumani na klabu ya Bayer Leverkusen, Karim Bellarabi.

Dortmund wamepata kikwazo cha uhamisho wa mchezaji huyo kutokana na mkazo uliowekwa na viongozi wa klabu ya Bayer Leverkusen, kwa kukataa ofa iliyowasilishwa siku kadhaa zilizopita.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Ruud Voller, amesema hawana mpango wa kumuachia Bellarabi kwa sasa, na wamedhamiria jambo hilo kikamilifu.

Hata hivyo Voller, amekiri kutumwa kwa ofa ya klabu hiyo ya Signal Iduna Park lakini maamuzi waliyonayo yamekua sababu ya kutolewa kwa jibu hilo.

“Tumepokea ofa yao kwa muda kidogo, lakini tumeikataa kutokana na hitaji letu kwa mchezaji huyu,”

“Kumuuza Karim sio mpango wetu kwa sasa. Na ninakuhakikishia ataendelea kubaki hapa.” Alisema Voller

Simba Waijibu Yanga Kuhusu Vuguvugu La ‘Hassan 'Kessy'
Video: Taarifa kutoka Wizara ya afya kuhusu mlipuko wa ugonjwa usiofahamika Dodoma