Meneja mpya wa klabu ya Man City, Pep Guardiola atakuwa mkuu wa benchi la ufundi la klabu hiyo, hata kama itashindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2016-17.

Meneja huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha mabingwa wa soka nchini Ujerumani, FC Bayern Munich tayari ameshasaini mkataba wa miaka mitatu wa kufanya kazi huko Etihad Stadium kuanzia msimu ujao wa ligi, kama mbadala wa Manuel Pellegrini atakaeondoka mwishoni mwa msimu huu.

Kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita kwa kukubalia kufungwa bao moja kwa sifuri na Man utd, kumeifanya Man city kujiweka njia panda ya kushiriki ama kutokushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Hatau hiyo ilizusha mjadala kwa wadadisi wa msuala ya soka barani Ulaya, kwa kuhisi huenda Pep Gurdiola akabadili maamuzi ya kuwa meneja wa Man city, kutokana na hitaji lake la kutaka kuona anakuwa sehemu ya mameneja ambao wataviongoza vikosi vyao katika michuano hiyo mikubwa barani humo.

Tangu alipoanza shughuli za kuvinoa vikosi vya klabu za FC Barcelona na kisha FC Bayern Munich, Guardiola hajawahi kukaa katika benchi la michuano ya ligi ya Europa (Europa League).

 

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) umebaini kwamba, hakuna sheria ama kifungu katika mkataba wa meneja huyo na uongozi wa Man city, ambacho kinaweza kumpa mwanya wa kuvunja makubaliano ambayo yameshasainiwa.

Klabu ambazo zinawania nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya nchini England, ambapo ndipo Man city walipo sasa ni West Ham Utd pamoja na Manchester United.

Jecha autaja uchaguzi mwingine wa Urais wa Zanzibar
Polisi Marekani wavamia nyumba ya Davido, wamhusisha na biashara ya ‘Unga’