Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer) ya Tanzania imeifunga Uganda mabao 7-5 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo Ijumaa Desemba 9, 2016 kwenye  Viwanja vya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri Sassii na mtunza muda, Idd Maganga mabao ya Tanzania yalifungwa na Samwel Opanga aliyefunga la kwanza, la sita na saba wakati mengine yalifungwa na Kashiru Salum, Ally Babby na Ahmada Abdi aliyefunga mawili.

Mabao ya Uganda yalifungwa na Emma Kalyowa aliyefunga bao la kwanza na la tatu wakati mengine walifungwa na David Kassa, Naturinda Ambrosse na Ochero Sulaimani.

Mchezo huo unaotambuliwa na CAF na FIFA, uliovutia mashabiki wengi wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ulilenga kuziandaa timu hizo kujiandaa na michuano ijayo ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la  CAF.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu amesema huu ni mwanzo mzuri wa kuiandaa timu yake na kufikia mafanikio ya juu katika soka la ufukweni hivyo kuwaomba wadau kuzidi kuwaunga mkono.

Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya  kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio.

Salome ya Diamond yawafunika Rihanna, J. Lo Kenya
Mchezo Wa Kirafiki Kuchangia Rambirambi Msiba Wa Ismail Khaflan