Kasumba ya mashabiki ya kutoonesha ushirikiano kwa baadhi ya wasanii Afrika mashariki, imemuibua mwanamuziki nyota wa miondoko ya Reggae Bebe Cool na kuzungumzia jambo hilo na kuwaomba mashabiki wa muziki kuonesha upendo na kuwanga mkono wasanii wa ndani kuliko wa nje ya mipaka ya mataifa yao.

Kauli ya Bebe cool imekuja kufuatia uungwaji mkono wa matamasha kadhaa ya wasanii wa Taifa hilo yaliyofanyika hivi karibuni yaliyofana kupita kiasi yakiwahusisha wanamuziki Juliana Kanyomozi, Azawi pamoja na B2C.

Hata hivyo, pamoja na kufana kwa matamasha hayo ya Uganda, bado nchi ya Nigeria imeendelea kutajwa kama mfano kutokana na wasanii wao kufanya vyema katika suala la kuungwa mkono na mashabiki wao wa ndani, jambo linaloongeza chachu ya wasanii hao kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya mipaka ya Taifa lao.

Mwanamuziki wa Uganda, Bebe cool.

Aidha, Bebe Cool ameweka wazi kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii nchini humo waliochoshwa na kufanya kazi kwa bidii bila kupewa sapoti wanayostahili, huku akitoa rai ya kutokuwapa kipaumbele wasanii kutoka mataifa kama Nigeria kabla ya kuwaunga mkono wasanii wa ndani.

Amesema, “Ninashukuru sana kwamba nyie mnaweza kujitokeza na tuna dada na kaka wanaofanya matamasha kila mahali nchini Uganda na ujumbe huu unaenda kwa vyombo vya habari na nendeni mkawaunge mkono wanamuziki wa Uganda.”

Bebe cool ameongeza kuwa, “tumechoka kufanya kazi kwa bidii bila msaada, kwanza niwashukuru waliohudhuria matamasha ya Azawi, Juliana na B2C, endeleeni kuwa na moyo kwani hilo ndilo litakalowatia moyo dada na kaka zetu kufikia pale wanapotaka.”

Mwimbaji wa muziki toka Uganda, Juliana.

Amesema, “Hatuwezi kuendelea kuwalaumu wanigeria wanafanya sehemu yao kwahiyo tufanye sehemu yetu sisi Waganda tupende muziki wetu na tuwasapoti wasanii wanaigeria, tunasapoti lakini sisi tupo hapa tunapambana nao! nani wamechukua Marekani? Tunahitaji kujifunza kutoka kwao, hivyo tuwaunge mkono ma-DJ, tuwaunge mkono ma-emcees, tuwaunge mkono wasanii. Tunahitaji kulipua mambo yetu.”

Nyota huyo, aliyarejea maoni aliyoyatoa mwimbaji Karole Kasita siku chache zilizopita alipozungumza kuwa Waganda hawaonyeshi mapenzi ya kutosha kwa wanamuziki wa ndani ya nchini hiyo kama ilivyo kwa mashabiki wa mataifa mengine dhidi ya wasanii wao.

“Nafikiri mashabiki wetu wanatakiwa kujifundisha kuwapenda wanamuziki wa hapa nyumbani bila kuwahukumu, huku wakiupenda muziki wao, kwa sababu waimbaji wa Uganda wanafanya kazi kwa bidii, wana muziki mzuri sana,” ameongeza Bebe cool.

Baada ya ligi kuu Parimatch yagawa upendo kwa wateja
Kenya: Odinga asema ataheshimu uamuzi wa Mahakama