Kuelekea katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa unaotarajia kupigwa leo baina ya Liverpool na Real Madrid kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Real Madrid, David Beckham amemuomba Zinedine Zidane kuhakikisha anawafunga Liverpool.

Inafahamika kuwa Beckham ni mpinzani wa Liverpool kwani alishawahi kucheza Manchester United na asingependa kuona wapinzani wake wakishinda mchezo wa leo dhidi ya Madrid.

”Imekuwa vizuri sana kupata mafanikio kama mchezaji na sasa kama kocha, namtakia mafanikio Zizou pamoja na rais wa klabu na chonde chonde naomba muwafunge Liverpool”,alisema Bekham.

Beckham na Zidane walicheza pamoja Real Madrid mwaka 2003 mpaka 2006 ambapo Zidane aliamua kustaafu kucheza soka.

Kama Zidane atafanikiwa kutwaa ubingwa leo atakuwa ameimeifikia rekodi ya makocha Carlo Ancelotti na Bob Paisley ambao wameshinda kombe hilo zaidi ya mara mbili.

Mara ya mwisho kwa Liverpool kutwaa ubingwa huo ilikuwa ni mwaka 2005 walipoifunga AC Milan kwa mikwaju ya penati na sasa wanawania ubingwa wa sita wa ‘Champions League’ mpaka sasa wakiwa tayari wametwaa ubingwa huo mara tano.

 

 

Video: Magufuli, Mkapa, Mangula siri nzito, DC amsweka ndani mwenyekiti CCM
Rushwa yazidi kuitafuna serikali ya Kenyatta