Waimbaji wa Kike wa Bongo Flava, Vanessa Mdee na Shilole wametibuana na kushindwa kuvumilia mipaka ya mgogoro wao na kuamua kuanikana kwenye mitandao ya kijamii.
Bifu hilo ambao limeanza kushika moto wiki hii, limekuwa kavukavu kwani kila mmoja amempost mwenzake kabla ya kumwaga matusi yake.
Ni kama kila mmoja ame-pick the wrong fight, Vanessa wa Uzunguni na Shilole anayejiita wa uswahilini, kila mmoja ana mtindo tofauti wa kumvuruga mwenzake.
Jana, Shilole amepost video na picha kadhaa zinazorusha makombora moja kwa moja kwa Vanessa Mdee akionesha kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kuchokozwa.
“Jaman Vee kaanzisha ugomvi Na wa Igunga ajue tu kuumaliza. Kukauka Kama kuni vepeeee #SayMaName” aliandika Shilole
“Veeee jipange Sana mwenzio IGUNGA niliaga cjaletwa kwa kubebwa kwenye Lori nimekuja Na mbio za mwenge. We c wa magorofan Na kingereza chako cha kuunga mi ndo mtoto wa mbwa sasa maninaaaaaaa,” alisema.
A photo posted by Shishi bybee /she roll it (@shilolekiuno_badgirlshishi) on
Naye Vanessa alishindwa kuvumilia na leo aliamua kurusha kombora akipost picha ya Shilole na kudai kuwa mwimbaji huyo anataka ampe ‘kick ajulikane’. Hata hivyo, Vanessa alidai kuwa Shilole hastahili post hiyo na kwamba angeitoa ndani ya muda mfupi.
“Nikupe KICKIII ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndiyo mtugaragaze. Sit the f**k down. Mimi sio wale uliowazoea. P.s: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi. #MessageSent” aliandika Vee Money kwenye post aliyoweka picha ya Shilole.