Serikali ya Canada imemzuia msanii wa Jamaica Beenie Man kuingia nchini humo kwa lengo la kufanya tamasha kubwa jijini Toronto linalojulikana kama OVO Fest, baada ya kubainika kupata maambukizi ya vizusi vya Zika.

Msanii huyo ameweka Instagram picha inayomuonesha akiwa katika hali ya maumivu kitandani akipata matibabu baada ya kukumbwa na virusi hivyo na kueleza kuwa ameshindwa kupewa Visa ya kuingia nchini Canada.

“No visa fi mi Canada show.  The same Zika mosquito gi mi dengue. Blood test, injections, pills. Wi a hol firm still,” aliandika.

Muandaaji wa tamasha hilo aliwaambia watu mashabiki waliokuwa wananunua tiketi kuwa Beenie Man hatakuwa mmoja kati ya watakaotumbuiza katika tamasha hilo kutokana na matatizo ya Uhamiaji.

Beenie Man amekumbwa na tatizo hilo ikiwa ni saa chache baada ya watu watu wanne kubainika kuwa na virusi vya Zika Kaskazini mwa Florida.

 

 

 

SSC Napoli Wapata Mbadala Wa Gonzalo Higuain
Jeremy Menez Arejea Ufaransa, AC Milan Wamuachia Kiulaini